
Zitto, Baba Levo wasaka rekodi Kigoma Mjini
Kigoma. Jimbo la Kigoma Mjini ni miongoni mwa majimbo yanayoibua mjadala na kufuatiliwa na wengi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025. Siku hiyo Watanzania wataamua nani atakayeshika hatamu za urais, ubunge na udiwani kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Macho mengi yanaitazama Kigoma Mjini, ambayo pia imekuwa midomoni mwa watu ambako historia, siasa na burudani…