Kessy alia utulivu African Sports
KICHAPO cha mabao 2-1, ilichokipata African Sports wiki iliyopita dhidi ya Stand United, kimemfanya kocha mkuu wa kikosi hicho, Kessy Abdallah kudai sababu zilizowanyima ushindi ni kutokana na wachezaji kukosa utulivu wa kumalizia nafasi. Kessy amezungumza hayo baada ya timu hiyo kupoteza michezo saba kati ya tisa iliyocheza baada ya kushinda mmoja na sare moja…