
Bado Watatu – 33 | Mwanaspoti
HAKUMALIZA sentensi yake akaninyooshea mkono wake na kukikunjua kiganja alichokuwa amekifumba. Akanionyesha kitu alichokuwa amekishika.Kilikuwa funguo ya gari la Shefa!“Hizi funguo ni za gari la Shefa na nimezikuta ndani ya pochi yako humu chumbani.”Mshituko nilioupata ulinifanya nitwete kama niliyekuwa nafukuzwa. Kumbe mume wangu aliichukua ile pochi na kuifungua, ndiyo maana niliikuta kitandani wakati mimi mwenyewe…