Mrundi aziingiza vitani Pamba Jiji, TRA United

LICHA ya beki wa kati wa Fountain Gate, Mrundi Derrick Mukombozi kubakisha mkataba wa miezi sita na kikosi hicho, ila timu mbalimbali zimeanza kuiwinda saini yake dirisha dogo la Januari 2026, zikiwemo za Pamba Jiji na TRA United. Mtu wa karibu na mchezaji huyo, ameiambia Mwanaspoti ni kweli nyota huyo anafuatiliwa na timu mbalimbali dirisha…

Read More

Atolewa uvimbe wa kilo tano tumboni alioishi nao miaka 10

Geita. “Nimezaa watoto 11 lakini mtoto wangu wa mwisho niliyemzaa mwaka 2010 nilikuwa nipoteze maisha, maana nilitokwa na damu nyingi sana, nikazimia mara tatu na wakati wote wa mimba damu ilikuwa inavuja, sikujua tatizo.” Haya ni maneno ya Eveline Paulo, mkazi wa Biharamulo mkoani Kagera aliyetolewa uvimbe wenye uzito wa kilo tano tumboni. Uvimbe huo…

Read More

Minziro kukwepa mtego wa play-off

KOCHA Mkuu wa Pamba Jiji, Fred Felix ‘Minziro’ ametoa siku 10 kwa wachezaji kabla ya kurejea kujiandaa dhidi ya JKT Tanzania na KMC akizitaja kama ndizo za kukwepa mtego wa kuangukia kucheza mtoano. Tayari Kagera Sugar na KenGold zilizopo nafasi ya 16 na 15 mtawalia zimeshuka Ligi Kuu na vita iliyobaki ni kucheza mtoano (play…

Read More

Wamachinga wanavyoitesa Serikali | Mwananchi

Dar/mikoani. Uamuzi wa Serikali kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga barabarani na kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyia shughuli zao, umeonekana kugonga mwamba. Hiyo ni baada ya makundi ya wafanyabiashara hao, kushuhudiwa yakirejea kwa kasi barabarani, huku ugumu wa biashara katika maeneo waliyopangiwa ukitajwa kuwa moja ya sababu. Kwa mujibu wa wamachinga wenyewe, kupangwa maeneo yaliyotajwa…

Read More

Sababu mashindano ya Quran kwa wanawake kufanyika Tanzania

Dar es Salaam. Haiba ya uadilifu, kupenda haki na usawa aliyonayo Rais Samia Suluhu Hassan, imetajwa kuchochea Tanzania ichaguliwe kuwa mwenyeji wa mashindano ya kwanza ya Quran kwa wanawake duniani. Mashindano hayo yamehusisha washiriki kutoka mataifa 11 duniani, ni mara ya kwanza kufanyika na Tanzania imekuwa mwenyeji wake. Hayo yameelezwa leo, Jumamosi Agosti 31, 2024…

Read More