WAFANYABIASHARA WA MTAA WA MAHIWA NA NZIGUA WAMLILIA MAMA SAMIA
UMOJA wa Wafanyabiashara wa Mahiwa na Nzigua wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati operesheni ya kuondoa wafanyabiashara wa kanzu, Mitandio pamoja na vitu mbalimbali vya maharusi wa dini Kiislamu katika barabara ya Mahiwa na nzigua. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Maadili Kasimu Kumbawene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam…