Mawakili walivyorushiana mpira, Dk Slaa kuendelea kusota mahabusu
Dar es Salaam. Wakati mwanasiasa maarufu nchini, Dk Wilbrod Slaa akiendelea kusota mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya jinai, mawakili wanaomtetea na mawakili wa Serikali wamerushiana mpira kila upande ukiutuhumu kuwa chanzo cha mwanasiasa huyo kupelekwa mahabusu na kuchelewesha kuamua hatima ya dhamana yake. Mawakili hao wamerushiana mpira huo, leo Alhamisi, Januari 23, 2025,…