
Uzembe barabarani ajali zaua 25 ndani ya wiki
Dodoma. Janga la ajali limezidi kuwa tishio nchini baada ya watu 25 kupoteza maisha katika matukio tofauti ndani ya wiki moja, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baadhi yao wakiwa mahututi. Ajali hizo zilitokea kwa nyakati tofauti katika mikoa tofauti, zikiwemo Pwani ambako watu watano wa familia moja walipoteza maisha juzi, Mwanza (watano), Mara (sita), na Dodoma…