
Umuhimu wa utekelezaji mkakati wa nishati safi ya kupikia
Dar es Salaam. Katika muktadha wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kimazingira, nishati safi imeendelea kuwa jambo la msingi kwa Taifa lolote linalotaka kupiga hatua kuelekea maendeleo endelevu. Nchi inayokumbwa na changamoto za kiafya, mazingira na umaskini, nishati safi ya kupikia si tu hitaji la msingi, bali ni kichocheo cha maendeleo ya kweli kwa watu…