Dk Biteko azindua bodi ya Tanesco akiagiza mambo sita
Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amezindua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), huku akitoa maelekezo sita. Miongoni mwa maelekezo hayo ni kuendeleza na kusimamia miradi ya kimkakati ya uzalishaji na usambazaji wa umeme ili kuhakikisha huduma ya umeme inaimarika na kuwafikia Watanzania wengi…