Maumivu ya bei yaja, usafirishaji kwenye meli juu
Dar es Salaam. Wakati kukiwa na malalamiko ya kupanda kwa bei za bidhaa za chakula kutokana na kupaa kwa mafuta ya dizeli na petroli, huenda kilio hicho kikaongezeka baada ya ongezeko kubwa la gharama za usafirishaji wa mizigo kwa meli. Sababu ya ongezeko hilo inaelezwa ni ukosefu wa usalama katika safari za meli zinazotoka Ulaya…