
Rais Mwinyi aifungua bandari kavu ya Maruhubi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mapinduzi makubwa katika sekta ya Miundombinu ya Bandari yanalenga kuifanya Zanzibar kuwa kituo muhimu cha Usafirishaji na kupokea Meli kubwa zinazoleta bidhaa nchini. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 18 Oktoba 2024 alipoifungua Bandari kavu ya Maruhubi, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amefahamisha…