
Kilio cha wananchi, stendi ya kisasa Kijangwani ikianza kufanya kazi
Unguja. Siku chache baada ya kuzinduliwa stendi kuu ya kisasa Kijangwani na kulazimisha daladala kupitia kwenye kituo hicho, wananchi na abiria wamelalamikia mzunguko mkubwa unajitokeza na kusababisha kero. Stendi hiyo ya kisasa ilizinduliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, Januari mwaka huu katika kuadhimisha miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuanza kufanya kazi…