UPANUZI WA KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO-K4 KUKIDHI MAHITAJI YA SUKARI NCHINI
Katika mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha nchi inakua na utoshelevu wa bidhaa ya Sukari, Kiwanda cha cha Sukari Kilombero kipo mbioni kukamilisha ujenzi wa upanuzi wa kiwanda chake cha K4. Kupitia mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika Agosti 1, Kampuni hiyo ilitangaza tukio kubwa la uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi…