Wanawake wahimizwa kuchangamkia fursa sekta ya usuluhishi
Dar es Salaam. Wakati sekta ya Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala (ADR) ikiendelea kukua kwa kasi duniani ikiwemo Tanzania, wadau wamewataka wanawake kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo kwani bado inatawaliwa zaidi na wanaume. Kwa mujibu wa takwimu za tafiti mbalimbali barani Afrika, asilimia 72 ya wasuluhishi ni wanaume huku wanawake wakiwa ni asilimia 28…