Msako ujenzi holela majengo Kariakoo waanza kung’ata
Dar es Salaam. Tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Mtaa wa Mchikichi na Congo, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 31 na kujeruhi wengine Novemba 2024, limeendelea kusalia kwenye vichwa vya Watanzania. Ni miongoni mwa matukio yaliacha taswira ya hofu ya usalama kwa kila mmoja anapolitaja eneo…