Polisi, RC, Chadema walivyojadili madai kutekwa Katibu wa Bavicha
Mwanza. Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza imekanusha tuhuma za kuhusika katika kutoweka kwa Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo ambaye inadaiwa alichukuliwa na watu waliojitambulisha ni maofisa wa polisi. Manengelo anadaiwa kutoweka Februari 14, 2025, akiwa nyumbani kwa rafiki yake wa kike, Pendo. Kamanda wa Polisi…