Mgombea wa Chadema aliyeenguliwa ashinda uenyekiti wa kijiji
Hai. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro kimeeleza kushangazwa na Mgombea wake katika Kijiji cha Useri, Kata ya Machame Narumu, Wilfred Ritte kutangazwa mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa kijiji hicho, licha ya kuondolewa katika kinyang’anyiro katika hatua za mapingamizi. Katika matokeo hayo mgombea huyo wa Chadema anaonekana kupata kura…