SERIKALI KUONGEZA KONGANI ZA VIWANDA KUIMARISHA UZALISHAJI

Serikali imepanga kuongeza maeneo maalum ya uwekezaji (kongani) nchini, hatua inayolenga kuchochea uzalishaji, kuongeza ajira na kuboresha mazingira ya kufanya biashara. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Tume ya Ushindani (FCC), Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, alisema sekta ya viwanda imeendelea kukua na kuimarika, hususan katika uzalishaji wa malighafi unaochangia maendeleo…

Read More

Uamuzi mgumu Yanga | Mwanaspoti

HESABU za Yanga kwa sasa hazipo sawa baada ya kupoteza mechi ya pili ya Kundi A katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikitishia tumaini la kucheza robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo, lakini tayari mabosi wa klabu hiyo akiwamo Kocha Sead Ramovic wamepanga kufanya uamuzi mgumu kwa timu hiyo. Yanga ilipoteza mchezo wa…

Read More

Mwili wa Tendwa waagwa, Kikwete aeleza alivyopigiwa simu

Dar es Salaam. Mwili wa John Tendwa aliyewahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini umeagwa leo, huku waombolezaji akiwamo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakieleza namna alivyoanzisha uhakiki wa vyama vya siasa. Wameeleza uhakiki huo ulipoanzishwa baadhi ya vyama havikuukubali lakini leo ndiyo uhai wa vyama vyote. Tendwa ambaye mwili wake utazikwa kesho Desemba 20,…

Read More

ZDCEA yanasa watano, kilo 798 dawa za kulevya

Unguja. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar (ZDCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imekamata kilo 798.89 za dawa za kulevya. Aina ya dawa zilizokamatwa katika operesheni maalumu nne tofauti zilizofanywa kuanzia Oktoba mwaka huu ni pamoja na bangi, cocaine, heroin, methamphetamine na shisha zilizochanganywa na dawa za…

Read More

Othman akerwa na Wasira, Mbeto kupotosha kuzuiwa kwao Angola

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman, ameeleza kushangazwa na upotoshaji uliofanywa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu kilichowatokea nchini Angola. Othman ameenda mbali zaidi na kutaka mamlaka zinazowasimamia ziwachukulie hatua kwa kile alichoeleza kuwa upotoshaji walioufanya unaipaka matope Serikali….

Read More