Sita kizimbani wakituhumiwa kumuua askari wa Tanapa
Geita. Watu sita wamepandishwa kizimbani wakishitakiwa kwa kosa la mauaji ya aliyekuwa askari wa Hifadhi ya Taifa (Tanapa), Julius Katambi, aliyeuawa Oktoba 20, 2023 akiwa lindo kwenye hifadhi ya Kigosi wilayani Mbogwe mkoani Geita. Washitakiwa katika kesi hiyo, namba 21464/2024, ni Mpandasabi Lutoja, Richard Mhozya (45), Mpejiwa Sumuni (35), Antony Sumuni (40), Majaliwa Marko (33)…