Serikali ya kijiji yawakatia bima wananchi wake Mbeya
Mbeya. Zaidi ya wananchi 1,500 katika Kijiji cha Mashese kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya wameondokana na gharama za matibabu baada ya serikali ya kijiji hicho kuwapatia bima. Bima hizo zinatokana na mapato ya ndani ambapo mbali na wananchi wa kawaida, pia, wanafunzi watanufaika na katika mpango huo unaolenga kuhakikisha jamii hiyo inakuwa salama…