WAZIRI MAKAMBA AWASILI NCHINI CHINA KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) leo tarehe 16 Mei 2024 amewasili nchini China kuanza ziara ya kikazi. Ziara hii mbali na kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia wa kihistoria uliopo baina ya mataifa haya mawili ni muendelezo wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ikilenga kufuatilia utekelezaji wa makubaliano…

Read More

TARI yaja na Utafiti wa Mbolea zinazotokana na taka

Mtafiti wa Udongo na Mbolea wa Kituo cha Serian Arusha Richard Temba akionesha Utafiti wa Mbolea unaotokana na taka ambazo baada ya uhifadhi zinazalisha minyoo ya kufanya uchakataji wa Mbolea ambapo Elimu ya Utafiti na Ubunifu ulitolewa katika Maadhimisho ya Elimu, Ubunifu na Ujuzi yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Popatlal Mjini Tanga….

Read More

Ujenzi wa nyumba Hanang wakamilika

Arusha. Tabasamu lakaribia kurejea. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya mawe, tope na miti kutoka Mlima Hanang yaliyotokea Desemba 3, 2023 wilayani Hanang mkoani Manyara. Kaya 108 zilizokosa makazi kutokana na maafa hayo zinatarajia kurejesha tabasamu tena baada ya ujenzi wa nyumba 108 zilizojengwa kwa ajili…

Read More

Makamu wa Rais mgeni rasmi Mei Mosi

Arusha. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewasili katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yanayofanyika kitaifa jijini humo. Awali Rais Samia Suluhu Hassan, alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo. Leo Mei Mosi, 2024 maadhimisho hayo yameanza  ambapo kwa sasa maandamano…

Read More

Ripoti yaibua mapya taka zinazooza Dar

Dar es Salaam. Wakati ripoti mpya ikionyesha asilimia 63.4 ya taka zinazozalishwa jijini Dar es Salaam ni zinazooza, wadau wameshauri kampeni za kukabiliana nazo ikiwa moja ya njia za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Taka hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na mabaki ya chakula na matunda, zinapooza hutoa gesijoto kama methane na kaboni,…

Read More

Dkt Biteko aungana na Wanabukombe kwenye mbio fupi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Doto Biteko leo Oktoba 10, 2024 ameungana na wananchi wa Bukombe kwenye mazoezi ya kukimbia mbio fupi za KM 5 ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwalimu Duniani ambayo yanafanyika Wilayani Bukombe, Oktoba 11, 2024. Mbio hizo zimehudhuriwa na…

Read More