SUA yaanza Maandalizi ya utafiti wa Mpunga Himilivu kwa mabadiliko ya tabianchi na rafiki kwa mazingira Africa.
Na: Calvin Gwabara – Morogoro Tanzania. Mradi wa Mpunga Himilivu kwa mabadiliko ya Tabianchi na Rafiki kwa Mazingira Barani Afrika (Climate-resilient and Eco-friendly Rice for Africa) (CERA) umechukua hatua muhimu katika kuboresha kilimo cha mpunga kwa kuendesha mafunzo maalum kwa wakusanyaji takwimu katika utafiti unaotarajia kufanyika kwenye Mikoa ya Morogoro, Shinyanga na Songwe nchini Tanzania….