BAADA YA SADC KUITAJA TANZANIA KINARA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA; KAMISHNA LUOGA ATAKA WATUMISHI KUKUZA MATUMIZI YA NISHATI HIYO
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amewataka Watumishi wa Wizara ya Nishati kuendelea kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini ili kufanikisha ajenda hiyo ambayo kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ameeleza kuwa ajenda ya nishati safi ya kupikia tayari imeanza kuonesha mafanikio…