
Bado Watatu – 31 | Mwanaspoti
NIKAUFUNGA ule mlango wa stoo. Tukaenda kukaa sebuleni.“Sasa nataka nikwambie kitu cha mwisho,” baba akaniambia, na kuongeza: “Hatujui nini kitatokea, lakini endapo utakamatwa, usikubali kuwa marehemu alikuja kwako kabla ya kuuawa. Hilo jambo likatae kabisa. Na hata kama namba za gari lako zitatajwa, pia usikubali wewe ndiye uliyekwenda kuitupa maiti yake. Sema namba za gari…